Vipengele 4 vya usimamizi bora wa hatari katika Deriv multipliers | Deriv Blog

Gundua zana unazoweza kutumia kwa usimamizi bora wa hatari katika biashara unapotumia Deriv multipliers.

Timu ya Deriv · 21 Julai 2022 · 2 dak kusoma

Share

Makala hii ilisasishwa tarehe 22 Januari 2024

Kufanya biashara kwa kutumia multipliers ni njia nzuri ya kuongeza faida yako inayowezekana. Katika majukwaa ya biashara ya Deriv, unaweza pia kuepuka hasara zinazoongezeka soko likikwenda kinyume nawe. Katika chapisho hili la blogu, tunaelezea jinsi vipengele vya usimamizi wa hatari kwenye majukwaa ya Deriv hufanya viwe chaguo bora kwa biashara ya multipliers.

Njia 4 Deriv inakupa udhibiti zaidi katika biashara yako ya multipliers 

Stop Out ya kiotomatiki 

Unapotumia multipliers kufanya biashara kwenye Deriv, huwezi kupoteza zaidi ya kiasi cha biashara yako. Kwa kipengele cha stop out ya kiotomatiki, nafasi zako hufungwa kiotomatiki mara tu hasara zako zikiwa sawa na kiasi cha biashara yako. 

Take Profit

Kwa kawaida, utahitaji kufunga nafasi yako mwenyewe ili kuhakikisha faida yako. 

Kipengele cha take profit kinakuruhusu kuendesha mchakato huu kiotomatiki. Unachotakiwa kufanya ni kuweka kiwango cha faida unachoridhika nayo. Ikiwa faida yako itafikia au kuongeza kiasi hiki, nafasi yako itafungwa na faida yako itaongezwa kwenye salio la akaunti yako. 

Stop loss

Stop loss inakuruhusu kuweka kiasi hasara unayotaka kupata. Unaweza kupunguza hasara yako kabla ya kupoteza kiasi chako cha biashara. 

Mara tu hasara yako ikiwa sawa au inazidi kiasi cha stop loss yako, biashara yako itafungwa kiotomatiki. 

Kwa mfano, unafungua biashara na kiasi cha biashara cha USD 10. Stop out ya kiotomatiki itafunga biashara yako hasara zako zikifika USD 10. Hata hivyo, ikiwa unataka kupunguza hasara zaidi, unaweza kuweka kiwango cha stop loss cha USD 5. Hasara yako ikifikia kiasi hiki, biashara yako itafungwa kiotomatiki.

Kughairi muamala

Umefungua biashara, lakini unakuwa na mashaka? Kwa kughairi muamala, una chaguo la kughairi biashara ndani ya kipindi kilichochaguliwa (kutegemea soko na kitu unachofanyia biashara) baada ya kufungua na kurudisha kiasi cha biashara yako. Tafadhali kumbuka kuwa Deriv inatoza ada ndogo kwa huduma hii.

---

Kwa hivi vipengele 4 vya usimamizi wa hatari, biashara ya multipliers kwenye Deriv inaweza kukusaidia kuepuka kupoteza fursa na kuzuia kupoteza zaidi ya ulivyo tayari kupoteza. Ingia au jisajili kwa akaunti ya demo bila malipo kujaribu Deriv multipliers. 

Join 3M+ global traders

Open an account in minutes and start trading the world's markets — forex, stocks, indices, and more.